Somalia na kuzidi ajira Ujerumani:
4 Januari 2007
Tukianzia na mada ya Somalia,gazeti la Saarbrücker Zeitung lasema kwamba,Umoja wa Ulaya umejiepusha na kila jaribio la kujifanya polisi wa dunia.
Waziri wa nje wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier,anabainisha dhahiri-shahiri kwamba kupeleka Somalia vikosi vya kuhifadhi amani huko ni jukumu la nchi za kiafrika.Bila shaka kusema hivyo sio kigeugeu.
Gazeti linasema:swali tu ni hili: kwa muda gani msimamo huo utabakia hivyo ?
Kwani talari yadhihirika kujiingiza huko kwa Marekani kunakobainisha kwamba huu nchini Somalia si mzozo wa Afrika tu.Hata Ulaya haiwezi kutojali kuwaona waislamu wenye itikadi kali wanaunda kambi mpya katika pembe ya Afrika.
Likiendelewza mada hii hii, gazeti la Sächsiche Zeitung kutoka Dresden linadai kwamba bila ya msaada kutoka nje ,Somalia haina nafasi ya kweli ya kuwa na mustakbala mwema.Kwamba Umoja wa Ulaya unafanya juhudi za kisiasa na kuimarisha juhudi za amani,kunastahiki kuungwamkono.
Hatahivyo, katika kikosi cha kusimamia amani cha kimataifa UU wala Marekani zisijiingize.Somalia haihitaji dola la kigeni kuikalia bali inachohitaji, ni msaada wa kuiungamkono serikali ya umoja wa Taifa.Na serikali ya aina hiyo, haiwezi kuundwa kwa kadiri nchini hali ya hofu, matumizi ya nguvu na kuto amaminiana imetanda.
Likitugeuzia mada gazeti la WESTDEUTSCHE ZEITUNG kutoka Düsseldorf linazungumzia juu ya kuendelea kupungua ukosefu wa kazi nchini Ujerumani na kuanza kustawi upya kwa uchumi:
Laandika:
“Idadi ya wasio na kazi kufuatana na msimu imeendelea kupungua na hii ni habari nzuri mwanzoni mwa mwaka mpya .
Bora zaidi ni kuona sambamba na hali hiyo kunazidi pia wafanyikazi wanaochangia ada zao katika bima ya jamii.Makampuni na viwanda vingi sasa vimeanza kutoa nafasi nzuri za kazi ,kwavile vinaona kustawi kwa uchumi si ‘msala upitao’ bali kutaendelea.
Ujerumani iko njia bora sasa kuparamia tena kileleni mwa dola za kiuchumi katika Umoja wa Ulaya.Serikali ya Ujerumani ambayo inafurahia mno hali hii,kwa kweli imepata bahati zaidi kuliko fahamu”- ni ya Westdeutsche Zeitung.
Gazeti la WESTFÄLISCHE POST kutoka Hagen linatupa macho katika soko jipya la ajira: Lasema:
“Upepo mzuri uliopiga katika soko la kazi- kunatokana na hali isio ya baridi kali ya hewa ambao umeendelea kubainisha uchumi unaanza kweli kuimarika.
Ishara hapa ni kuzidi kupungua watu wasio na kazi ambako si tukeo la kimaumbile bali kunatokana na juhudi kubwa zilizochukuliwa na nchi nyingi za kiviwanda –miongoni mwa juhudi hizo na mageuzi yaliokwishafanywa naserikali ya Kanzela Schröder.
Juu ya hivyo, kushangiria sasa ni mapema.Swali ni kuwa:ndio watu zaidi wamerudi makazini,lakini hali zao kulingana na mahitaji ya viwanda na kampuni zimebadilika mno.
Kujipatia kazi za mikataba ya kudumu,salama wa kubakia na kazi kuweza kudiriki kuwa na famiglia na kununu vitu madukani kunazidi kuwa jambo adimu.” Lasema Westfalempost kutoka Hagen.
Sawa na gameti hilo STUTTGARTER NACHRICHTEN laonya:
„Ikiwa wanasiasa watagutuka haraka kuridhika na hali ya mambo,mambo yaweza yakageuka nayo haraka na kuwa kama yalivyokua zamani-kwavile, kustawi uchumi daima kunaambatana na mikondo 2:Haitakua mara ya kwanza kwa wanasiasa ghafula baada ya mafanikio ya kwanza ,wakaanza kuregeza kamba.
Mkondo huu unaelekeza wapi ,mtu aliweza kujionea kipindi kirefu cha enzi ya utawala wa Bw.Schröder.Majaribio hayo basi hayahitaji tena kukaririwa.“
Likitukamilishia uchambuzi huu,gazeti la hapa Bonn-General Anzeiger laonya hivi:
„Jambo moja makisio haya ya kuwa uchumi unarudi kustawi mwanzoni mwa mwaka mpya lisitudanganye. Kwani, kazi nyingi zinazochangia ada katika mfuko wa bima ya jamii zimetokana na makampuni ya kazi za muda maalumu.Na kama nafasi hizo zilivyoibuka haraka,zaweza kutoweka haraka.“