Somalia kuisaidia Somaliland baada ya soko kuteketea moto
4 Aprili 2022Matangazo
Roble amesema fedha hizo ni msaada wa kimataifa uliotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya jimbo la Somaliland ambalo lilijitangazia uhuru wake kutoka kwa Somalia.
Viongozi wa wafabiashara wa Somaliland pia wameahidi kuchangia ili kusaidia kulijenga upya soko hilo.
Rais wa Somaliland, Muse Bihi Abdi amesema amezungumza kwa njia ya simu na Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo na Waziri Mkuu Roble kuelezea masikitiko yao kutokana na moto huo.
Kundi la al-Shabaab lenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda, pia yameelezea kusikitishwa na moto huo. Meya wa Hargeisa, Abdikarim Ahmed Mooge amesema wafanyabiashara katika soko hilo wamepoteza mali yenye thamani ya dola bilioni mbili.