Klabu ya kwanza ya soka ya wanawake Somalia iitwayo Golden Girls Centre huko Mogadishu, inalenga kuvunja miko na kusaidia kuwapa mafunzo ya soka wasichana ili wawe wachezaji wa kulipwa. Kuwaona wasichana wakicheza soka Somalia ni jambo la nadra sana kutokana na shinikizo za kijamii na hofu ya kundi la kigaidi la Al-Shabaab.