Soka: Werder yaikaribia Schalke kileleni.
19 Machi 2007Matangazo
Nchini Ujerumani , Werder Bremen imeilazimisha Mainz kusalim amri kwa mabao 2-0 na kusogea karibu na viongozi wa ligi daraja la kwanza nchini Ujerumani Bundesliga Schalke 04, kwa tofauti ya points tatu.
Katika pambano lingine jana Jumapili Bayer Leverkusen imeipiga mweleka Borussia Monchengladbach iliyoko mkiani mwa Bundesliga kwa bao 1-0.