Soka. Werder warejea kileleni.
3 Desemba 2006Matangazo
Nchini Ujerumani, Werder Bremen imerejea kileleni tena katika ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Hertha BSC Berlin.
Mabingwa watetezi Bayern Munich walipata sare ya bao 1-1 dhidi ya Borrusia Mönchengladbach.
Katika michezo mingine Borussia Dortmund imeizaba Wolfsburg kwa bao 1-0 na Hanover imerejea matokeo kama hayo dhidi ya Cottbus.
Bielefild na Leverkusen walitoka sare ya bila kufungana .
Na katika mpambano wa timu zilizoko katika eneo la kushuka daraja Bochum iliichapa Hamburg kwa mabao 2-1.