Soka. ManU waangukia pua.
5 Aprili 2007Matangazo
Katika michezo miwili ya duru ya kwanza ya michezo ya robo fainali katika kinyang’anyiro cha kombe la mabingwa la vilabu barani Ulaya , jana jioni kumekuwa na michezo miwili. As Roma ya Italia imeigaragaza Manchester United ya Uingereza kwa mabao 2-1 wakati Valencia ya Hispania ikiwa ugenini imeilazimisha Chelsea ya Uingereza kutoka sare ya bao 1-1 katika uwanja wa Stanford Bridge.