1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Soka. Chalsea yasonga mbele katika kinyang’anyoro cha Champions League Ulaya.

13 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFNo

Katika soka jana usiku, timu pekee ya Ujerumani Bayern Munich iliondolewa katika kinyang’anyiro cha ligi ya mabingwa, champions League, licha ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Chalsea ya Uingereza.

Chalsea inasonga mbele katika nusu fainali kwa jumla ya mbao 6-5.

Wakati huo huo mpambano mwingine wa robo fainali kati ya mahasimu wa jadi Inter Milan na AC Milan ulikatishwa katika dakika ya 73 baada ya mlinda mlango wa AC Milan Mbrazil Dida kupingwa na kitu kinachowaka moto uwanjani. Katika wakati huo Inter ilikuwa nyuma kwa bao 1-0. Chama cha kandanda barani Ulaya UEFA kitaamua iwapo mchezo urudiwe ama AC Milan ipewe ushindi katika mchezo huo.