Sissi aioya Ethiopia juu ya mzozo wake na Somalia
22 Januari 2024Matangazo
Sissi ametoa matamshi hayo siku ya Jumapili (Januari 21) katika ziara ya Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia nchini humo na kuongeza kuwa Ethiopia isiijaribu Misri wala kuwatishia ndugu zake na hasa ikiwa watawaomba kuingilia.
Rais huyo wa Misri ametoa matamshi hayo baada ya Ethiopia kutangaza kwamba inaweza kulitambua jimbo lililojitenga la Somaliland kuwa taifa huru.
Hii ni kufuatia makubaliano baina yao yanayoiruhusu Ethiopia kutumia bandari na kuanzisha kituo cha kibiashara na jeshi la maji katika ukanda wa pwani kwenye Ghuba ya Aden kwa miaka 50 ijayo.
Sissi, ambaye amesema Misri haitaruhusu Ethiopia "kukiuka uhuru wa ardhi ya Somalia," ameikosoa Addis Ababa juu ya namna inavyolichukulia eneo hilo lililojitenga.