SINGAPOUR: Singapour inavunja rikodi ya hukumu za kifo, yasema Amnesty International.
15 Januari 2004Matangazo
Ripoti maalum ya shirika la kutetea haki za binaadamu Amnesty International kuhusu kisiwa cha Singapour, inasema zaidi ya watu mianne wamehukumiwa adhabu ya kifo na wakanyongwa kisiwani humo, kati ya mwaka wa 1991 na mwaka wa 2003. Kiongozi wa tawi la shirika hilo kwa ajili ya Singapour na Malaisia, Bibi Margaret John, amesema idadi hiyo inazusha wasiwasi mkubwa, katika nchi ambayo wakaazi wake wanakadiriwa kuwa zaidi kidogo ya miliyoni nne. Shirika hilo linasema hukumu zinatolewa katika mazingira ya kutatanisha; na linawatolea mwito wakuu wa Singapour, kupiga marufuku hukumu ya kifo. Likiitaja ripoti ya shirika la umoja wa mataifa miaka ya nyuma, Amnesty International linasema kati ya mwaka wa 1994 na mwaka wa 1999, Singapour ilivunja rekodi ya hukumu za kifo duniani, kwa kuwa idadi ya watu waliohukumiwa adhabu ya kifo, ilikuwa zaidi ya asilimia 13 ya raia wote. Shirika la Amnesty International linasema zaidi ya nusu ya watu hao waliohukumiwa adhabu ya kifo, walikuwa wageni.