1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SINGAPORE: Vijana wapatiwe elimu na mafunzo ya kazi

16 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDBh

Benki Kuu ya Dunia imetoa wito wa kuongezwa misaada ya kuwapatia vijana elimu na mafunzo ya kazi katika nchi zinazoendelea.Vijana bilioni 1.3 kati ya umri wa miaka 12 na 24 wanaoishi nchi zinazoendelea,lazima wapewe uwezo wa kuwa na maisha bora au kutazuka hatari ya kuongezeka kwa mivutano ya kijamii.Wito huo umetolewa kwenye mkutano wa kila mwaka wa Benki Kuu ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF,ulioanza hii leo nchini Singapore.Kufuatia lawama zilizotolewa na jumuiya ya kimataifa,Singapore imeondosha vikwazo vya usafiri vilivyowekwa dhidi ya wanaharakati 22 wanaopigania haki za binadamu na kukosoa mfumo wa masoko huria duniani.Hapo awali kiongozi wa Benki Kuu,Paul Wolfowitz aliilaumu Singapore kuwa inajidhuru kwa kutumia mabavu.