1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Simba wamechacha Ethiopia

20 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEZG

Addis Ababa:

Simba wakikasirishwa na kuharibiwa kwa misitu wamewaua watu 20 na kula mifugo yao 750 nchini Ethiopia. Afisa wa wilaya ya Soro iliyoko umbali wa km 500 kusini mwa mji mkuu, Addis Ababa, Bw. Tadesse Gichore, amesema kuwa mashambulio hayo yanayofanywa mchana, yamewalazimisha Wakulima kadhaa kuhama nyumba zao na kuwawinda simba hao wala watu. Simba wamewala Wachungaji waliokuwa wanachunga ng’ombe na Wanavijiji baada ya kuvunja nyumba zao. Bw. Gichore amesema kuwa watu elfu kadhaa waliohisi kuwa maisha yao yamo hatarini wameacha nyumba zao na kukimbilia kwenye usalama mwezi uliopita. Simba walioanza kurandaranda baada ya makazi yao ya misituni kuharibiwa na kusababisha ukame katika Bonde la Mto Gibe, sasa wanawindwa.