1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya mwisho ya Uchaguzi wa Wabunge nchini Rwanda

19 Septemba 2008

Nchini Rwanda uchaguzi wa wabunge umakamilika.Katika hatua ya kihistoria Rwanda limekuwa taifa la kwanza ulimwenguni kuwa na idadi kubwa zaidi ya wanawake bungeni kwa mujibu wa matokeo ya muda.

https://p.dw.com/p/FLKX
Raia wa Rwanda apiga kura yakePicha: picture-alliance/ dpa

Wanawake wamejinyakulia viti 44 jambo linalowawezesha kuwa na uwakilishi mkubwa bungeni.Kwa kujibu wa takwimu za Chama cha ushirikiano wa mabunge IPU idadi hiyo imeipiku nchi ya Sweden iliyo na asilimia 47 ya wanawake bungeni na Cuba iliyo na asilimia 43 ya wabunge wanawake.Chama tawala cha Rwandan Patriotic Front, RPF kinaripotiwa kuwa mstari wa mbele katika uchaguzi huo wa wabunge.Huu ni uchaguzi wa pili kufanyika tangu mauaji ya halaiki kutokea mwaka 1994.

Kutoka Kigali John Kanyunyu ana maelezo zaidi.