Siku ya mwisho ya kampeni Ufaransa
5 Julai 2024Matangazo
Muungano wa vyama vya mrengo wa kati unaoongozwa na Rais Emmanuel Macron umekubaliana kuachiliana viti na muungano wa mrengo wa kushoto ili kukizuwia chama cha siasa kali za mrengo wa kulia kinachoongozwa na Marine Le Pen kushinda kwenye uchaguzi huo.
Soma zaidi: Vyama vya kihafidhina vyashikilia viti vingi bunge la Ulaya
Ikiwa muungano wa Le Pen utashinda viti 289 kati ya 577 vya bunge, wataweza kuunda serikali itakayoongozwa na mshirika wake, mwenye umri wa miaka 28, Jordan Bardella, kama waziri mkuu.
Ghasia na mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya wagombe na wanasiasa yamekuwa yakiripotiwa, huku wizara ya mambo ya ndani ikisambaza zaidi ya maafisa 30,000 wa polisi kukabiliana na matukio hayo.