1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waingereza bado wamechanganyikiwa

21 Oktoba 2016

Katika siku 100 tangu aanze kazi kama waziri mkuu wa Uingereza, utendaji kazi wa Theresa May umekuwa wa kuvutia kumzidi mtangulizi wake japo bado ana kibarua kikubwa juu ya maridhiano ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/2RXJP
London Downing Street Theresa May
Picha: picture-alliance/dpa/A. Rain

Katikati ya mwezi Julai, Theresa May alianza kufanya kazi kama waziri mkuu wa nchi hiyo akiwa ni waziri mkuu wa 54. Alichukua wadhifa huo wakati chama chake cha Kihafidhina kikiwa katika msukosuko kutokana na hofu iliyosababishwa na matokeo ya kura ya maoni juu ya Uingereza kutokuendelea kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Kampeni kuelekea kura hiyo ilisababisha maumivu na kuweka wazi udhaifu wa chama hicho ambacho kwa miaka mingi kimekuwa na mgawanyiko kuhusu suala la Ulaya.

May, ambaye sasa amekuwa katika nafasi hiyo kwa siku 100, amechukuwa hatua muhimu kuhusu suala hilo akilinganishwa na mtangulizi wake, David Cameron.

"Kumekuwa na uwezekano wa kuchukua hatua kuhusu sera ya siasa na filosofia ya Cameroon," anasema Oliver Pantel, mtafiti katika Taasisi ya Ulaya katika Chuo Kikuu cha London.

"Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, wanachama kutoka chama cha Kihafidhina walichaguliwa kwa kusudi maalumu, na kura ya kujitoa Umoja wa Ulaya imetumika kama kama moja kati ya kusudi hilo ili kuelekea upande mwingine kabisa, licha ya kuwa kura hiyo ilikuwa ni kuhusu Umoja wa Ulaya. Kitu hicho hakikutakiwa kutokea katika demokrasia", anaongeza mtafiti huyo

Udhaifu wa wapinzani wamsadia 

Pamoja na hayo, hali ya kutokujiweka sawa katika chama cha Labour, ambacho kimetumia muda mwingi katika miezi mitatu iliyopita kuzozana katika uchaguzi wake wa ndani, inamaanisha kuwa May amekutana na upinzani mdogo.

"Nadhani nguvu zake ziko nje wa uwezo wake na ni wapinzani. Anasaidiwa sana na upinzani dhaifu pengine zaidi ya waziri mkuu mwingine yeyote yule," anasema Matthew Cole, mhadhiri wa Historia katika Chuo Kikuu cha BirminghamMay, ambaye anasisitiza kuwa asingelipenda Ulaya itoe tafsiri ya nafasi yake, juhudi zake na ajenda yake havionekani kuwaingia wapigakura wa kawaida.

London EU Referendum Brexit Symbolbild
Moja ya bango kuhusu kujitoa Umoja wa UlayaPicha: Getty Images/AFP/P. Faith

Chochote ambacho May anatamani, swali kubwa linaliokabili serikali ni jinsi gani hasa kutafanyika utekelezaji wa matokeo ya kujitoa Umoja wa Ulaya.

Alipoulizwa kuhusu msimamo wake wa sasa, Waziri Mkuu huyo ambaye mwenyewe alipiga kura ya  kubaki katika Umoja huo, alisisitiza kuwa "kujitoa Umoja wa Ulaya maana yake ni kujitoa Umoja wa Ulaya."

Katika mkutano wa chama chake, May alitangaza kuwa Kifungu cha 50 kitaanzisha mazungumzo mnamo mwisho wa Machi 2017. Katika hotuba yake alikiri kuwa "kujitoa kugumu" maana yake ni kujitenga na Umoja wa Ulaya na hii inajumuisha pia soko la pamoja.

Watu wengi nchini Uingereza wamechanganyiwa. Hawajui nini kitafuata baadaye.

Mwandishi: Celina Mwakabwale/DW English

Mhariri: Mohammed Khelef