Wakati utawala wa Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukitimia siku 100, wananchi na wachambuzi wanajiuliza ikiwa ameanza na dalili njema au naye ni muendelezo wa utawala wa takribani miaka 40 wa Chama chake cha Mapinduzi (CCM) ulioshuhudia ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma ukishamiri na kuzorota kwa hali ya maisha.