Siddi: Waafrika waliosahaulika India
Watu 25,000 wa jamii ya Wabantu wa Afrika Mashariki wamekuwa wakiishi katika misitu ya Ghatis ya Magharibi mwa India. Mababu wa jamii hiyo ya Siddi kwa kiasi kikubwa walifikishwa India kama watuzmwa.
Namna ya kipekee ya muziki na uchezaji
Jamii ya Siddi inastawi kupitia nyumba zao za asili na ngoma. Ni sehemu muhimu ya utambulisho wa utamadaduni. Manuel ni mkulima katika wilaya ya Kamataka Uttar. Katika wakati wa mapunziko, Manuel anafanya warsha ya ngoma kwa watoto kwa kuendeleza utamaduni wa Siddi kwa kizazi kijacho.
Hand-crafted instruments
Mwalimu anawafundisha watoto katika kijiji cha Mainalli namna ya kupiga ngoma, Chomba ambacho kimetengenezwa kwa mti na ngozi ya wanyama. Kwa kawaida, wanaume hupiga ngoma na wanawake wanacheza midundo ya kuvutia.
'Dhamal'
Binti wa miaka 13 Chandrika anajiandaa kwa dhamal, ngoma ya asili ya Siddi. Dhamal ni ngoma inayoeleza maosha ya Siddi. Chandrika anaishi katika kijiji cha Mainalli na anapenda kwenda shule pamoja na kujifunza mambo yahusuyo dhamal.
Ngoma kwa ajili ya mfalme
David pia akijiandaa kwa kucheza dhamal. Ngoma ya kiasili ambayo ambayo ilikuwa ikichezwa baada ya mafanikio ya uindaji. Dhamal pia ilikuwa kiburudisho kwa mfalme kwa siku za nyuma. Lakini katika kipindi hiki inachezwa katika hafla mbalimbali.
Bonded labor
Watengeneza wa filamu wanaandaa eneo kwa ajili ya vipindi vya TV, "Sentuhan Harapan." Katika picha hii, wanaigiza simulizi ya Ravi. Ravi ni mfanyakazi aliyefungwa na kupigwa na mfanyabiashara wa eneo hilo. Wakati Ravi alikataa kufanya kazi kwa mshahara wa duni, mfanyabiashara pia alishambuliwa na familia ya Ravi.
Uonevu mashuleni
Kijani mwanafunzi wa jamii ya Siddi mjini Yellapur anaonesha uzoefu wake wa unyanyasaji na uonevu akiwa shuleni ikiwa ni sehemu ya "Sentuhan Harapan." Mwanafunzi anasema kwa kawaida watoto wengine hawataki kuwa na maingiliano na watoto wa jamii ya Siddi, jambo linalowaafanya watoto wengi wa jamii hiyo kuacha shule.
Upotaji wa ardhi
Mahadevi ni mjane wa umri wa miaka 75 anaeishi katika kijiji cha Magod. Mahadevi anaendelea kuhakikisha anashinda kesi ya kurejesha katika himaya yake eka tano za aridhi ambayo iliporwa kinyume cha sheria na afisa ardhi, kufuatia kifio cha mumewe 1996.
Muda wa mapumziko
Kundi la wasichana kutoka jamii ya Siddi wanachenza katika mti wa zamani kijijini kwao Mainalli, wakibembea katika matawi yake.Kikiwa kizazi cha watu wa Afrika Mashariki kutoka jamii ya Wabantu, mababu wa Siddi walifikishwa India kama watumwa na Waarabu mwanzoni mwav karne ya 7, na kufuatiwa na Wareno na Waingereza baadaye. Wengine walikwenda India kufanya kazi kama wafanyabiashara au mabaharia.
Nelson Mandela ni shujaa kwa jamii ya Siddi
Picha ya rais wa kwanza na mpinga ubaguzi wa rangi Nelson Mandela imepachikwa katika ukuta wa nyumba moja ya familia ya jamii ya Siddi katika kijiji cha Talkumbri. Wakati biasahara ya utumwa ilipopigwa marufuku, Jamii ya Siddi ilikimbilia katika misitu ya India, kwa kuhofia kukamatwa na kuadhibiwa. Kwa karne kadhaa watu 25,000 wa wa asili ya Afrika wamekuwa wakiishi katika hali isiyotambulika.