SICILY: Wahamiaji haramu wawasili visiwani Sicily, Lampedusa na Crete
29 Agosti 2005Wahamiaji haramu 500 wamewasili kwa njia ya madau katika visiwa vya Sicily na Lampedusa na kisiwa cha Ugiriki cha Crete. Dau lililotia nanga huko Agrogent, Sicily, lilikuwa limebeba watu wengi zaidi ya idadi linalotakiwa kubeba. Wengi wa abiria wote 150 wanatokea mashariki na magharibi mwa Afrika. Mara tu walipowasili walipelekwa hospitalini kwa sababu ya uchovu.
Mbali na kisiwa cha Crete walinda usalama waliwatia mbaroni wahamiaji wengine 150 na watu wawili wanaofanya biashara ya kuuza watu. Licha ya juhudi za umoja wa Ulaya kuwazuia wahamiaji kuingia Ulaya kwa njia ya madau, wengi huingia barani humu karibu kila siku hasa wakati wa kiangazi. Walinda usalama wa Itali wanasema wafanyibiashara wa kuuza watu wanatumia madau madogo ili kukwepa kukamatwa.