1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siasa na uchumi wa Italia uko matatani

9 Novemba 2011

Bei za hisa za makampuni katika masoko ya Ulaya zimeshuka pakubwa na kusababisha Italia kujaribu kuunda serikali ya mseto itakayoifufua hali ya uchumi nchini humo.

https://p.dw.com/p/137ky
Waziri mkuu wa Italia, Silvio BerlusconiPicha: dapd

Tayari wawekezaji nchini Italia wana hofu kubwa kuwa nchi hiyo iko njiani kuelekea katika mzozo wa madeni ya Ulaya, kutokana na deni lake kubwa la trillioni 2.6 Mmoja wa wawekezaji nchini humo amsema kwa sasa wana wasiwasi kwa sababu Italia inapitia kipindi kigumu, kisiasa na pia kiuchumi, na hadi sasa hakuna msimamo dhabiti juu ya swala hili.

Muekezaji huyo amesema hajui serikali itakayoundwa itawajumuisha akina nani na itakuwa serikali ya vipi na iwapo wataweza kweli kuitanzuwa hali ilivo kwa sasa.

Bei za hisa katika masoko ya ulaya Zimeshuka kwa asilimia 2.1, ikiwa katika pointi 963.2 Wataalamu wa mambo ya kiuchumi wanasema hali hii inaweza kuiweka Italia katika mzozo mkubwa wa madeni.

Kwa upande wake, waziri mkuu, Silvio Berlusconi, amesema leo kwamba atajiuzulu pindi tu bunge litakapoidhinisha sheria ya kuufufua uchumi wa nchi hiyo, ilioshinikizwa na washirika wake walio wanachama wa Umoja wa Ulaya itakayosaidia katika kupata suluhu juu ya mzozo wa madeni unaotishia nchini humo.

Hatua ya kuidhinisha sheria hiyo inatarajiwa kufanywa mwezi huu. Hata hivo, chama cha waziri mkuu Berlusconi kimeitisha uchaguzi katika kupatikana atakayechukua nafasi hiyo, huku upande wa upinzani ukitaka kuundwe serikali ya umoja wa Taifa itakayoongozwa na mtaalamu wa mambo ya uchumi.

EU Finanzminister Brüssel
Wanachama wa Umoja wa UlayaPicha: dapd

Waziri mkuu wa Finland Jyrki Katainen na waziri wa fedha wa Austria, Maria Fekter, wote wameonya kuwa Italia, kati ya nchi tajiri katika bara la Ulaya, inaonekana kuwa kubwa mno kupokea msaada, ikilinganishwa na mataifa mengine kama  vile Ugiriki katika kupokea misaada ya kulipia madeni yake. Wawili hao wamesema wanashindwa kuelewa namna Italia itakavyosaidiwa katika deni lake.

Umoja wa Ulaya una wasiwasi mkubwa juu ya hali ilivyo nchini Italia na tayari umoja huo uko nchini Italia kuangalia marekebisho ya maswala muhimu ya uchumi baada ya umoja huo na shirika la kimataifa la fedha duniani, IMF, kuiweka Italia katika uwazi wa kuichunguza juu ya mpango wake wa kuinua uchumi.

Kwa sasa Umoja wa Ulaya unajitahidi katika kusaidia Italia iwapo itahitaji msaada wakati huu ambapo inakabiliwa na msukosuko wa kisiasa na kifedha. Baada ya Ugiriki, Ireland na Portugal sasa Italia ni ambayo ni ya tano katika nchi kumi na saba za Umoja wa Ulaya inaelekea pabaya katika maswala yake ya kiuchumi, hasa baada ya kukataa mkopo wa euro billioni 50 kutoka kwa shirika la kimataifa la fedha duniani IMF.

Mwandishi Amina Abubakar/RTRE/AFPE

Mhariri: Othman, Miraji