Shirikisho la kandanda Uhispania lamtaka Rubiales ajiuzulu
29 Agosti 2023Matangazo
Shinikizo hilo limetokana na kitendo cha kumbusu midomoni mchezaji, Jenni Hermoso kwenye Kombe la Dunia.
Shirikisho hilo la kandanda la nchini Uhispania limechukua hatua hiyo wakati hali inazidi kutifua mzozo wa kitaifa kuhusu haki za wanawake.
Wakati huo huo kaimu mawaziri kadhaa wanamshauri Rubiales aondoke.
Hapo awali wawakilishi wengi wa shirikisho hilo walimpongeza Rubiales alipotangaza siku ya Ijumaa kuwa hatajiuzulu lakini hali imebadilika.
Jumatatu walimtaka aachie ngazi na pia wanataka mabadiliko yafanyike katika nyadhifa mbalimbali kwenye shirikisho la kandanda nchini Uhispania.
Shirikisho kuu la vyama vya soka duniani,FIFA tayari limemsimamisha Rubiales.