Shirika la biashara la kimataifa WTO litaongozwa na mwanamke kwa mara ya kwanza katika historia yake baada ya Ngozi Okonjo-Iweala wa Nigeria na Yoo Myung-hee wa Korea Kusini kufuzu kwa duru ya tatu na ya mwisho ya mchakato wa kumpata Mkurugenzi mtendaji mpya wa shirika hilo.