Shirika la ujasusi la CIA latakiwa lijieleze
17 Desemba 2007Matangazo
Afisa mkuu wa chama cha Republican katika kamati ya bunge inayohusika na maswala ya ujasusi, ameupuuza utawala wa rais George W Bush na kuahidi kuchunguza kisa cha kuharibiwa kwa kanda za uchunguzi za shirika la ujasusi la CIA.
Peter Hoekstra amesema anataka shirika la CIA libebe dhamana na lieleze wazi kilichotokea kuhusu kanda hizo za uchunguzi. Idara ya sheria ya Marekani imelitaka bunge lisichunguze kisa hicho na kuwashauri maafisa wa ujasusi wasishirikiane na maafisa wa kamati ya bunge watakaochunguza kashfa hiyo.
Mapema mwezi huu shirika la ujasusi la Marekani, CIA, lilitangaza kwamba liliziharibu kanda za video zinazoonyesha maafisa wa kundi la al Qaeda wakihojiwa kwa ukali.