1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiEthiopia

Shirika la ndege la Ethiopia lakabiliwa na changamoto

28 Julai 2023

Shirika la ndege la Ethiopia, ambalo ni shirika pekee barani Afrika linaloingiza faida, bado linakabiliwa na changamoto kadhaa ukiwemo uagizaji wa vipuri vya ndege zake.

https://p.dw.com/p/4UV9b
Äthiopien Ethiopien Airlines
Picha: Kola Sulaimon/AFP/Getty Images

Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo la ndege la Ethiopia, Mesfin Tasew amewaeleza waandishi wa habari wa AFP kwamba wanakabiliwa na kesi iliyowasilishwa na shirika moja la kutetea haki za binaudamu juu ya madai ya ubaguzi dhidi ya wasafiri kutoka jimbo la Tigray.

Tasew ameongeza kwamba shirika lake lilipata faida kubwa katika kipindi cha janga la UVIKO-19, na pia mwaka wa fedha wa 2022-2023 ulikuwa wa mafanikio makubwa.

Shirika hilo linalomilikiwa na serikali liliingiza dola bilioni 6.1, likiwa ongezeko la asilimia 20 ikilinganishwa na mwaka uliopita na ongezeko la karibu asilimia 50 ya mapato yaliyopatikana kabla ya janga la UVIKO-19.