Shirika la kazi duniani ILO laadhimisha miaka 100
11 Aprili 2019Suala la vijana kukosa ajira pamoja na wahamiaji linatoa changamoto mpya kwa shirika hilo la ILO linapotimiza miaka 100 tangu kuundwa kwake. Wakati shirika hilo likitimiza miaka 100 tangu kuundwa tarehe ya leo , bado shirika hilo halijafikia malengo yake .
Jana Alhamis tarehe 11 mwezi Aprili shirika la kazi duniani ILO lilisherehekea miaka 100 tangu kuanzishwa. Tangu mwanzo kabisa mradi huu ulikuwa na mtazamo wa dhamira kuelekea , serikali , waajiri , vyama vya wafanyakazi na shirika la ILO kwa pamoja kuweka viwango vya usawa kazini duniani kote , na wakati huo huo kuhakikisha utekelezaji wa hali hiyo.
Kwa kuwa wenye mkampuni na wawakilishi wa serikali hawataki kabisa kushiriki katika utekelezaji wa mada hii ya usawa wa kijamii katika Umoja wa Mataifa, hali ilivyokuwa katika wakati wa vita vikuu vya kwanza ndio iliyoweza kufanikisha hilo. Katika kivuli cha mapinduzi nchini Urusi yanayojulikana kama mapinduzi ya Oktoba mwaka 1917 vuguvugu la wafanyakazi lilipata ushawishi mkubwa. Bila ya mafanikio ya vyama vya wafanyakazi amani katika bara la Ulaya isingekuwapo.
Kwa hakika ILO inapaswa kutazama kuhusu baadhi ya mafanikio na mageuzi muhimu , anasema Benjamin Luig kutoka Wakfu wa Rose-Luxembourg na kukumbusha juu ya kuwekwa sheria ya haki ya kukusanyika katika suala la uchumi unaohusiana na kilimo mwaka 1921.
Mwanzoni mwa mapinduzi ya viwanda wafanyakazi wa mashambani walifanyishwa kazi kama watumwa, ameeleza Luig. Pia katika sekta ya kilimo shirika la ILO katika miaka ya 1990 mpango wake uliporomoka.
Luig anakosoa kwamba ILO wakati huo ilitumbukia katika wimbi la uliberali mamboleo, katika kile kinachojulikana kama kuunga mkono mpango wa kuoanisha na mifumo mingine na kuuamini, ambao unaongozwa na masoko.
Lakini katika miaka iliyopita shirika la ILO lilijihusisha zaidi katika nyanja ya watoto kufanyishwa kazi pamoja na hali ya maeneo ya kufanyia kazi, amesema Luig.
Shirika la ILO binafsi halitapenda kuangalia nyuma yale yaliyotokea katika wakati huu wa maadhimisho yake ya miaka 100, badala yake linatazama kazi zilizoko mbele yake, linataka mabadiliko katika Umoja wa Mataifa kuhusiana na hali ya maeneo ya kufanyia kazi na hata Afrika , anasema Peter Van Rooij , mkurugenzi wa ofisi ya ILO nchini Nigeria. Ukosefu wa kazi kwa vijana ni changamoto kubwa. Afrika ni bara changa na mafunzo na elimu ni muhimu, ameeleza vanRooij katika mahojiano na DW.
Kwa vijana kuweza kuwapa mwelekeo kunahitaji mambo mengi. Vijana wengi zaidi wanakosa kazi , mara waingiapo katika umri wa kufanyakazi.
Matokeo yake, wanapoaua kutafuta kazi vijana wengi kutoka bara hilo hukimbia nchi zao, idadi kubwa wanakuwa wakimbizi wa kutafuta kazi.
Rooij anasisitiza kuwa tunapaswa kuwa na msimamo wa dhati katika kufanyakazi kwa pamoja na viwanda na mataifa ambayo vijana wanakimbilia. Sio kupuuza ujuzi wa wahamiaji , na kwamba ni muhimu kwa baadhi ya nchi kuutambua.
Vijana ni mtaji wa mabara yote, kwa hiyo ILO inapaswa kutilia maana uwezo wa vijana na kuutilia maanani kwa kiasi kikubwa, na kuwasaidia baadhi ya wale , ambao wanataka kujitegemea.