1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yasema ubaguzi unaofanywa na polisi hauripotiwi

10 Aprili 2024

Shirika la haki za msingi la Umoja wa Ulaya - FRA limetoa wito wa mageuzi ya kukomesha ubaguzi wa rangi katika idara za polisi barani Ulaya ikiwa ni pamoja na ukusanyaji bora wa data ili kulifanyia tathmini tatizo hilo.

https://p.dw.com/p/4edP1
Frankreich | Proteste gegen Polizeigewalt in Paris | Ausschreitungen
Shirika la haki la Umoja wa Ulaya lasema ubaguzi unaofanywa na polisi hauripotiwi vilivyoPicha: Olivier Arandel/MAXPPP/dpa/picture alliance

Katika utafiti wake wa kwanza wa kina kuhusu ubaguzi wa rangi katika idara za polisi barani Ulaya, FRA, imesema imegundua kuwa watu wa asili tofauti ya kikabila hukabiliwa na matamshi ya ubaguzi na hata vurugu.

Miongoni mwa mapendekezo yake, ni ukusanyaji bora wa data.

Ripoti hiyo ya utafiti wa FRA imesema kuwa mataifa mengi ya Ulaya hayakusanyi data rasmi za visa vya ubaguzi wa rangi vinavyowahusisha polisi ama hawana rekodi nzuri ya data hizo.

FRA imeongeza kuwa kukosekana kwa data ya kitaifa kunafanya kuwa vigumu kutathmini ukubwa wa tatizo hilo na kuweka taratibu za kulitatua.

FRA imesema kuwa ni Ujerumani , Jamhuri ya Czech na Uholanzi pekee zinazochapisha data hizo mara kwa mara ama kunapotolewa ombi.