1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sheria ya ugaidi yazusha upinzani tena Kenya

13 Machi 2007

Sheria ya kupambana na ugaidi inajadiliwa tena motomoto nchini Kenya .yafuatia onyo la Marekani kwa wasafiri kabla mbio za ubingwa wa nyika mjini Mombasa baadae mwezi huu.

https://p.dw.com/p/CHID

Wakereketwa wa haki za binadamu wameimarisha kampeni yao dhidi ya sheria inayopangwa kupitishwa kupambana na ugaidi.

Hii inafuatia onyo kwa wasafiri liliotolewa na Marekani kuhusu uwezekano wa kuzuka shambulio la kigaidi nchini Kenya wakati wa mashindano ya mwezi huu ya ubingwa wa mbio za nyika ulimwenguni-World cross-country championship huko Mombasa,Kenya.

Mwambi Mwasaru,mkurugenzi mkuu wa Tume ya Haki za binadamu nchini Kenya-kikundi kisicho cha kiserikali amenukuliwa kusema,

“hatuungimkono ugaidi,lakini acha vita dhidi ya ugaidi viendeshwe kwa njia inayoheshimu haki za binadamu.” Mwisho wa kumnukulu.

Zaidi ya watu 200 wameuwawa na kiasi cha 5.000 wamejeruhiwa katika ile hujuma ya mwaka 1998 katika Ubalozi wa marekani mjini Nairobi na shambulio jengine wakati mmoja mjini Dar-es-salaam,Tanzania.

Hujuma hizozikafuatiwa na shambulio jengine 2002 katika mwambao wa Kenya wa mombasa pale bomu ndani ya motokaa liliporipuka ndani ya hoteli mali yamuisrael.

Visa hivyo vyote jukumu lilitwikwa mabegani mwa Al Qaeda.

Sheria ya kupiga vita ugaidi iliochapishwa mwaka 2003 nchini Kenya inaruhusu mtuhumiwa ugaidi kuwekwa kizuizini bila mashtaka kwa muda usio na kikomo pamoja na kupokonywa mali yake miongoni mwa vifungu vyengine vya sheria hiyo.

Vyama vinavyotetea haki za binadamu vikavaa njuga kuipinga sheria hiyo,lakini iliibuka tena kujadiliwa Oktoba mwaka jana wakati wa mkutano uliojumuisha wakereketwa na mabingwa wa kisheria.Wakereketwa wa haki za binadamu wanadai sheria hii bado inakiuka haki za binadamu na sasa wamepania kupambana nayo tena.

Pakiwepo au pasiwepo sheria ya kupiga vita ugaidi,jinsi washukiwa ugaidi wanavyoandamwa sasa nchini Kenya tayari ni hali inayotia wasi wasi.

Januari mwaka huu, polisi wa Kenya waliwatia nguvuni zaidi ya watu 70 kwa tuhuma tu za ugaidi.Sehemu kubwa ya watu hao waliwekwa korokoroni kwa kiasi cha mwezi mmoja kinyume na sheria isemavyo.

Baadhi yao si wakenya na jamaa zao hawakujua hali zao na walipo-alisema Bw.Kimathi,mkurugenzi wa chama cha haki za binadamu nchini Kenya.

Sheria hivi sasa inaruhusu mtuhumiwa kuwekwa kizuizini kwa muda usiopindukia masaa 24 au kwa kosa kubwa, si kwa zaidi ya wiki 2 kabla kuhukumiwa mahkamani au kuachwa huru.

Mashindano ya ubingwa wa mbio za nyika ulimwenguni-world cross-country championship huko Mombasa,Machi 24 yxanatazamiwa kuwaleta pamoja wanariadha kutoka nchi 66 mbali mbali duniani.

Kenya imetoa maanani onyo lililotolewa na Marekani juu ya usalama .Isitoshe, serikali ya Kenya imeliandikia shirikisho la riadha ulimwenguni-IAAF kulihakikishia kwamba kwamba hatua za ulinzi zimechukuliwa kuhakikisha mbio hizo za nyika zinafanyika kwa amani.hii imetokana na shirikikisho hilo kuuliza juu ya usalama.

Mwaka jana,Marekani ilitoa onyo sawa na hilo pale maalfu ya wajumbe kutoka kila pembe ya dunia, walipofunga safari ya Nairobi kuhudhuria mkutano juu ya mabadiliko ya hali ya hewa.