Wabunge wa upinzani nchini Tanzania Jumanne (07.02.2017) walitoka bungeni kwa kile walichokieleza kuwa Naibu spika wa bunge kwenda kinyume na sheria ya kinga, madaraka na haki za bunge kutokana na kukamatwa kwa wenzao wa Arusha na Kilombero. Je, kanuni za bunge zinasemaje kuhusu hili? Caro Robi alizungumza na mwanasheria wa kituo cha sheria na haki za binadamu Tanzania, Harold Sungusia.