1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Picha 5
Utamaduni
22 Juni 2017
https://p.dw.com/p/2f82M

Je Yoga ni nini?

Ni aina ya zoezi la kiafya linalozingatia namna ya kudhibiti upumuaji, kuweka viungo vya mwili katika namna tofautitofauti huku ukitafakari kuhusu jambo. Zoezi hili hufanywa kwa manufaa ya kiafya na kutuliza akili na mwili. Kulingana na historia, zoezi hili lilianza na jamii ya Wahindi. Kadhalika kwa wanaolienzi, inaaminika kuwa ni zoezi linalowaunganisha washiriki na Mungu. Katika miaka mitatu iliyopita, zoezi hili lilianza kusherehekewa kote ulimwenguni na kutengewa Juni 21 kuwa tarehe yake maalum kusherehekewa kimataifa. Hii hapa baadhi ya picha ya jinsi sherehe zilivyokuwa katika sehemu chache za ulimwengu.