1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBangladesh

Sheikh Hassina ashinda muhula wa tano Bangladesh

8 Januari 2024

Waziri Mkuu wa Bangladesh ameshinda muhula wa tano madarakani na chama chake kimejizolea robo tatu ya viti bungeni katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana Jumapili ambao hata hivyo ulisusiwa na chama kikuu cha upinzani.

https://p.dw.com/p/4ayKS
Uchaguzi wa bunge Bangladesh
Mpiga kura akishiriki zoezi la uchaguzi BangladeshPicha: Mohammad Ponir Hossain/REUTERS

Tangazo lililotolewa mapema hii leo na tume ya uchaguzi ya Bangladesh limeonesha chama cha Hassina cha Awami League kimeshinda kwa wingi mkubwa uchaguzi huo uliowavutia asilimia 40 pekee ya idadi jumla ya wapigakura.

Soma pia: Vibanda vya kupigia kura vya chomwa moto Bangladesh 

Tume hiyo imesema chama hicho kimepata viti 223 lakini kufuatia ushindi wa wanasiasa wengine wenye ushirikiano na chama cha Awami, serikali ya Hassina itakuwa na wingi mkubwa kwenye bunge lenye viti 300.

Chama kikuu cha upinzani cha Bangladesh Nationalist (BNP) kiliususia uchaguzi huo kikiutaja kama "hadaa" na kuitisha mgomo wa nchi nzima dhidi ya utawala wa Sheikh Hassina ambaye anakosolewa kwa kuwakabili wapinzani kwa mkono wa chuma.