SHARM EL-SHEIKH: Israel kuachilia huru wafungwa 250 wa Fatah
26 Juni 2007Matangazo
Waziri Mkuu wa Israel,Ehud Olmert ametangaza mpango wa kuwaachilia huru wafungwa 250 wa chama cha Fatah cha Rais wa Wapalestina,Mahmoud Abbas. Olmert alitoa tangazo hilo mwishoni mwa mkutano wa kilele wa pande nne uliofanywa katika mji wa kitalii wa Sharm el-Sheikh nchini Misri.Mbali na Olmert na Abbas,mkutano huo ulihudhuriwa pia na Mfalme Abdallah wa Pili wa Jordan na mwenyeji Rais Hosni Mubarak wa Misri.Hadi Wapalestina 10,000 wapo katika jela za Israel.