1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SHANNON, Ireland :Uturuki,Iraq na Marekani kushirikiana kupambana na PKK

2 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7AY

Marekani ,Uturuki na Iraq zinatangaza kushirikiana kwa pamoja ili kupambana na waasi wa kundi la PKK wanaendeleza mashambulizi yao dhidi ya Uturuki kutokea eneo la kaskazini mwa Iraq.Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi Condoleeza Rice hakufafanua kauli hiyo.Bi Rice alikuwa mwanzoni mwa ziara yake ya Uturuki na Mashariki ya Kati na kuonya dhidi ya vitendo vitakavyochochea hali katika mataifa hayo mawili.Mashambulizi yamesababisha vifo vya waTuruki 47 mpaka sasa wakiwemo wanajeshi 35 tangu mwishoni mwa mwezi wa Septemba.Serikali ya Uturuki kwa upande wake inatisha kushambulia eneo la kaskazini mwa Iraq endapo Marekani na maafisa wa serikali ya Iraq hawatachukua hatua za kuwadhibiti waasi wa PKK.Hapo jana Uturuki ilianza kutekeleza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya kundi la waasi la PKK ili kuyumbisha shughuli zao.

Juhudi za kidiplomasia zinashika kasi ili kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Bi Condoleeza Rice ameshawasili nchini Uturuki ili kukutana na viongozi wa nchi hiyo.Uturuki bado haijabadili msimamo wake.