1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Shambulizi la Droni la Ukraine laua watu 6 Urusi

6 Mei 2024

Shambulizi la droni la Ukraine dhidi ya mabasi mawili yaliyokuwa yakiwapeleka watu kazini, limewaua watu 6 na kuwajeruhi watu wengine 35 katika mkoa wa Urusi wa Belgorod.

https://p.dw.com/p/4fXbL
Mkoa wa Belgorod umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara
Mkoa wa Belgorod ambao unapakana na Ukraine, umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara kwa makombora na ndege zisizo na rubani za Ukraine katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.Picha: Belgorod Region Governor/dpa/picture alliance

Gavana wa mkoa huo Vyacheslav Gladkov, amesema shambulizi hilo limetokea karibu na kijiji cha Berezovka.

Ameongeza kuwa mwanaume mmoja yuko katika hali mbaya na watoto wawili wamepata majeraha makubwa.

Mkoa wa Belgorod ambao unapakana na Ukraine, umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara kwa makombora na ndege zisizo na rubani za Ukraine katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Ukraine imekuwa ikikanusha kuwalenga raia na kuongeza kuwa inayo haki ya kuishambulia Urusi.

Moscow nayo inasema nchi za Magharibi zinapuuza mashambulizi ya Ukraine dhidi ya raia.