1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la Bomu lamuua jenerali wa jejshi Lebanon

12 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CagJ

BEIRUT.Kumetokea mlipuko mkubwa wa bomu karibu na makazi ya rais huko Lebanon ambapo watu wanne wameuawa akiwemo afisa wa ngazi ya juu katika jeshi la nchi hiyo, Brigadier General Francois el Hajj.

Brigadier Francois el Hajj ambaye alikuwa ni mkuu wa kitengo cha harakati katika jeshi, ni miongoni mwa watu waliyokuwa wakitegemewa kumrithi Generali Michel Suleiman nafasi ya ukuu wa majeshi iwapo generali Suleiman atachaguliwa kuwa rais.

Jeshi la nchi hiyo limetoa taarifa fupi kuthibitisha kuawa kwa General Francois pamoja na mlinzi wake.

Shambilizi hilo limetokea baada ya hapo jana bunge kuahirishwa kwa mara ya nane kupiga kura ya kumchagua rais hali inayoashiria mvutano mkali miongoni mwa wanasiasa.

Kuna wasi wasi kuwa huenda kuahirishwa huko kukaendelea hadi mwezi March mwakani.