Shambulizi laua, kujeruhi Wapalestina wakisubiri msaada Gaza
29 Februari 2024Haya ni kwa mujibu wa maafisa wa hospitali ya eneo hilo. Daktari Jadallah Shafai, mkuu wa idara ya wauguzi katika hospitali ya Shifa, ameiambia televisheni ya Al Jazeera kuwa karibu watu 50 wameuawa na 250 kujeruhiwa. Hakutoa idadi kamili ya vifo na majeruhi.
Televisheni hiyo imerusha video inayoonyesha miili kadhaa na watu waliojeruhiwa wakiwasili katika hospitali ya Shifa. Jeshi la Israel limesema linazichunguza ripoti hizo.
Soma pia: UN: Watu 576,000 wanakabiliwa na hatari ya kutumbukia kwenye baa la njaa ukanda wa Gaza
Hayo yanajiri wakati wapatanishi kutoka Misri, Qatar na Marekani wakipendekeza kusitishwa vita hivyo kwa muda wa wiki sita.
Wanatumai kwamba makubaliano hayo yanaweza kuanza mwanzoni mwa mwezi mtukufu kwa Waislamu wa Ramadhan ambao unatarajiwa kuanza Machi 10 au 11, kulingana na kuandama kwa mwezi kwa mujibu wa kalenda ya Kiislamu.