Shambulio la kujitoa mhanga laua kadhaa Kabul
15 Januari 2008Matangazo
KABUL:
Shambulio la kujitolea mhanga katika hoteli moja ya kifahali katika mjini mkuu wa Afghanistan- Kabul- limewauwa watu wasiopungua 6 na kuwajeruhi wengine 6. Wapiganaji wa Kitaliban wamejigamba kuhusika na shambulio hilo.Shambulio hilo limekuja wakati wa ziara ya waziri wa mashauri ya kigeni wa Norway-Jonas Gahr Store.Store anasemekana hakujeruhiwa. Polisi inasema kuwa washambuliaji wawili waliwarushia maguruneti walinzi wa hoteli hiyo wakati walipoingia kwa nguvu katika hoteli hiyo kabla ya kujilipua.