1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulio la Kabul

Hamidou, Oumilkher28 Aprili 2008

Wataliban wavuruga gwaride la kijeshi mjini Kabul

https://p.dw.com/p/Dpsr
Rais Hamid Karzai anusurika na shambulio la watalibanPicha: AP



Njama iliyoshindwa ya kutaka kumuuwa rais Hamid Karzai wa Afghanistan,bei ya mafuta ya petroli na,mijadala kuhusu mishahara ya viongozi wa mashirika na makampuni makubwa makubwa humu nchini ni miongoni mwa mada zilizomulikwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.


Tuanzie lakini Afghanistan ambako gwaride la kijeshi kuadhimisha miaka 16 tangu wanajeshi wa Urusi walipoihama nchi hiyo,lilikua nusra ligharimu maisha ya rais Hamid Karzai.Magezti mengi yalitupia jicho hali ya mambo nchini Afghanistan,mfano wa SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linalohisi ni dhahiri:


"Wataliban wamedhihirisha jinsi serikali ilivyodhaifu.Kishindo ni kikubwa kinachomkabili rais.Kwasababu wananchi walimchagua kwa sababu moja tuu:nayo ni ile ahadi ya kurejesha usalama na nidhamu nchini.Hakuna kinachowavunja moyo zaidi waafghan  kuliko kuona kwamba ahadi zilizotolewa hazitekelezwi-hakuna kinachowafanya wasiimaini serikali kuliko hilo.Ndio maana Hamid Karzai analazimika kila siku kupigania uhai wake,na sio tuu wa kisiasa."


Hayo ni maoni ya gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG.Die HEILBRONNER STIMMER linahofia:


"Lingekua balaa kubwa kwa mataifa ya magharibi.Wangefanikiwa wataliban na mpango wao wa maangamizi basi jumuia ya kimataifa ingekabiliwa na kizungumkuti kikubwa.Tangu Marekani ilipompandisha madarakani Hamid Karzai,mipango yote ya kurejesha amani nchini humo imeandaliwa kwa kuzingatiwa kua yeye ndie anaesalia kua rais.Hakuna wa pili.


Nalo gazeti la THÜRINGER ALLGEMEINE linahisi:


Hata maadhimisho hayo hayasaidii kuwaleta pamoja wataliban na serikali.Gwaride la jadi mjini Kaboul limemalizika kwa mizinga na risasi kufyetuliwa.Kila upande umeonyesha nguvu zake za kijeshi.Bila shaka Karzai amejaribu kufifiisha nguvu za shambulio la wataliban.Lakini hata kama yeye na mabolozi wa nchi za nje hawakujeruhiwa,wataliban lakini wamefanikiwa kurejea tena midomoni."


Gazeti la DER NEUE TAG linaandika:


"Aibu kubwa hiyo kwa Karzai.Hata katika mji mkuu,wanakokutikana wanajeshi elfu tatu,hayuko salama.Kinachotia uchungu zaidi ni vile wanajeshi walivyotimka ,kila mmoja akitapia maisha yake,wataliban walipoanza kushambulia.Picha hizo zinabainisha Karzai bado haidhibiti hali ya mambo miaka sita baada ya kukabidhiwa madaraka.


Sasa tuiingilie mada ya pili magazetini:kupanda mno bei ya mafuta ya petroli.Gazeti la WESTDEUTSCHEN ZEITUNG linaandika:


Ikiwa bei ya mafuta itaendelea kupanda kwa kasi hivi,basi wenye magari makubwa makubwa watajikuta siku moja wakilazimika kulipa mamia ya yuro ili kujaza magari yao.Kwa hivyo ni jambo linaloingia akilini  madareva wa magari wanaposhukuria kila pendekezo linalotolewa la kupunguza bei ya mafuta.Wanasiasa wanaitambua hali hiyo,wanajua,wakitaka kujiipatia umaarufu,wanabidi waitumie fursa iliyojitokeza."


Kwa upande wake gazeti la MÜNCHNER MERKUR linaandika:


Serikali ndiyo inayochochea kupanda bei ya mafuta na gesi.Ingekua hakuna malipo ya kodi za mapato,basi bei ya mafuta ya petroli ingesalia kua centi 59.Kwa hivyo lingekua jambo la maana kama serikali ingewarejeshea walipa kodi angalao sehemu ya mabilioni ya fedha inayochota.




►◄