Kenya imepata hasara ya dola milioni moja katika kipindi cha mwaka wa kwanza tangu kuzinduliwa kwa reli ya kisasa kutoka Nairobi kwenda Mombasa, ijulikanayo kama SGR, mradi unoafadhiliwa na serikali ya China.
https://p.dw.com/p/31jdl
Matangazo
MMT-J2 19.07 Kenia SGR and the Kenyan loss - MP3-Stereo
Serikali ya China imeijenga reli hiyo kwa mkopo wa dola bilioni 3, utakaolipwa kwa kipindi cha miaka 15 ijayo. Wanauchumi wanakadiria kuwa China inaidai Kenya asilimia 70 ya deni jumla la taifa. DW imezungumza na mwanauchumi Charles Karisa, kwanza anaelezea tathimini yake ya hasara ambayo Kenya imepata kupitia mradi wa SGR.