SEVILLE: Mawaziri wa ulinzi wa NATO wajadili mkakati mpya
8 Februari 2007Matangazo
Mawaziri wa ulinzi wa nchi zilizo katika Shirika la kujihami la magharibi NATO,hii leo wanakutana nchini Hispania,kuujadili mkakati mpya wa kijeshi kuhusu Afganistan.Washirika wa NATO wana hofu kuwa katika kipindi cha majuma yajayo,waasi wa Kitaliban wataanzisha mashambulio mapya,hali baridi ya hewa itakapoanza kubadilika.Waziri wa ulinzi wa Marekani,Robert Gates anatazamiwa kuutumia mkutano huo kuwahimiza wanachama wengine wa NATO kupeleka vikosi zaidi nchini Afghanistan ambako tayari kuna wanajeshi 33,000.