1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SEVILLA:mawaziri wa ulinzi wa jumuiya ya NATO wajadili Afghanistan

8 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUC

Mawaziri wa ulinzi wa nchi za NATOwanakutana leo mjini Sevilla nchini Uhispania kujadili jukumu la majeshi yao nchini Afghanistan.

Kitovu cha majadiliano hayo ya siku mbili ni matayarisho ya mkakati wa kukabiliana na wapiganaji wa kitalibani.

Wadadisi wa masuala ya kijeshi wanaamini kuwa NATO inahijataji askari zaidi ili kuweza kutekeleza jukumu la kulinda amani nchini Afghanistan.

Mkutano huo ni wa kwanza ambapo waziri wa ulinzi wa Marekani bwana Robert Gates atashiriki.