Sevilla yashinda Kombe la Ligi ya Ulaya kwa kuifunga Roma
1 Juni 2023Gonzalo Montiel, aliyefunga penalti ya mwisho na ya ushindi wa Argentina katika fainali ya Kombe la Dunia la FIFA dhidi ya Ufaransa, alitia kimiani penalti ya ushindi baada ya wachezaji wa Roma Roger Ibanez na Gianluca Mancini kukosa penalti zao.
Mechi hiyo ilikamilika sare ya 1-1 katika muda wa kawaida huku Roma ikitangulia kufunga bao dakika ya 35 ya mchezo kupitia kiungo Paulo Dybala kabla ya Sevilla kusawazisha kunako dakika ya 55.
Klabu hiyo ya Uhispania, sasa imeshinda fainali zote saba walizocheza katika mashindano hayo huku nahodha Jesus Navas akiwa miongoni mwa wachezaji waliopata ushindi wao wa kwanza dhidi ya Middlesbrough mwaka 2006.
Ushindi huo unaifanya Sevilla kufuzu kwa mashindano ya Ligi ya mabingwa msimu ujao licha ya kumaliza nje ya timu nne bora ndani ya La Liga.