1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Umoja wa Kitaifa yaundwa Tunisia

Kabogo Grace Patricia18 Januari 2011

Waziri Mkuu wa Tunisia, Mohamed Ghannouchi ametangaza kuunda serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa katika matumaini ya kurejesha utulivu nchini humo.

https://p.dw.com/p/zyza
Waziri Mkuu wa Tunisia, Mohamed GhannouchiPicha: AP

Waziri Mkuu huyo na mawaziri wa mambo ya nje, mambo ya ndani na ulinzi wataendelea kubakia katika nyadhifa zao, huku wizara kadhaa zikiwa zimegawiwa kwa wanachama wa upinzani.

Maandamano makubwa kupinga ukosefu wa ajira yaliyopamba moto mwezi huu, yamesababisha mauaji ya wazu 78 na kuondoka madarakani kwa rais wa muda mrefu Zine El Abidine Ben Ali, aliyekimbilia Saudi Arabia Ijumaa iliyopita.

Kwenye mji mkuu wa Tunis, jana polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya karibu waandamanaji elfu moja waliokuwa wanadai kuachia madaraka viongozi wengine wote wa chama tawala. Maandamano hayo yalichochewa na taarifa kuwa Ben Ali ameondoka nchini humo na tani 1.5 za dhahabu.