1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya umoja wa kitaifa Libya yapata msukumo mpya

6 Aprili 2016

Juhudi za kimataifa za kuumaliza mzozo nchini Libya na kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa zimepata msukumo mpya baada ya serikali iliyokuwa imejitangazia madaraka mjini Tripoli kutangaza kuachia mamlaka

https://p.dw.com/p/1IQ6f
Libyen Tripolis Fayez Serraj Einheitsregierung
Picha: Getty Images/AFP/Str

Hayo yanakuja ikiwa ni chini ya wiki moja baada ya kuwasili mjini humo, viongozi wa serikali ya umoja wa kitaifa. Hata hivyo ilikuwa haijawa wazi kama taarifa yake hiyo ya maandishi ilikuwa inaungwa mkono na mawaziri wote wa serikali hiyo ya uwokozi. Hatua hii inachukuliwa kama moja ya hatua za kuipa nafasi serikali ya umoja wa kitaifa kuwa na mamlaka kamili baada ya miaka kadhaa ya kuwapo na tawala mbili hasimu.

Mataifa ya magharibi yameonesha imani kwa serikali hiyo inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kuwa itasaidia kudhibiti kitisho kinachoasababishwa na wanamgambo wa kundi la Dola la Kiisilamu nchini humo, kuzuia wahamiaji ambao wanatumia njia ya Mediterrania kuvuka na kuingia barani Ulaya na pia kufufua uchumi wa nchi hiyo kwa kuimarisha sekta ya uzalishaji wa mafuta.

Libyen Regierung Konflikte
Waziri Mkuu mtarajiwa wa Libya Fayez Serraj akiongoza kikao cha Baraza la RaisPicha: picture alliance/dpa

Viongozi wa serikali hiyo ya Umoja wa kitaifa waliwasili kwa njia ya meli wakitokea nchini Tunisia jumatanoiliyopita, baada ya serikali hiyo ya uwokozi iliyokuwa imejitangazia madaraka kufunga anga ya Tripoli ili kuwazuia wajumbe wa serikali hiyo ya umoja wa kitaifa wasiweze kutumia usafiri wa ndege kuingia katika mji wa Tripoli.

Kwa mujibu wa afisa mmoja wa wizara ya sheria nchini humo, taarifa ya serikali hiyo ya uwokozi imekuja mnamo wakati mawaziri wakikutana kwa ajili ya kuandaa utaratibu wa kukabidhiana madaraka kwa njia za amani. Afisa huyo alisema taarifa hiyo ilikuwa na muhuri wa serikali ingawa haikuwa na jina au saini ya mawaziri.

"Taarifa hiyo ilisema " kutokana na imani tuliyo nayo katika kuupa umuhimu kipaumbele cha taifa na pia kuokoa damu ya Walibya tunachukua nafasi hii kukuarifu kuwa tumeamua kujivua madaraka tuliyo nayo ambayo ni pamoja na madaraaka ya Rais, mawaziri na manaibu waziri wa serikali iliyokuwepo" ilisema taarifa hiyo.

Taarifa za kujiuzulu kwa serikali hiyo ya uwokozi nchini Libya zimepongezwa na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika mgogoro huo wa Libya Martin Kobler ambaye saa chache kabla alikuwa mjini Tripoli kwa ajili ya kukutana na Fayez Serraj, ambaye ni kiongozi wa baraza linaloungwa mkono na Umoja wa Mataifa ambalo lina jukumu kubwa la kusimamia ustawi wa serikali hiyo ya umoja wa kitaifa. Aidha akizungumza na maafisa serikali hiyo ya umoja wa kitaifa nchini humon mjumbe huyo maalum wa Umoja wa Mataifa alisema:

Serikali hiyo ya uwokozi nchini Libya ilishika madaraka baada ya muungano wa makundi yenye silaha kushinda mapambano kwa ajili ya udhibiti wa mji wa Tripoli mnamo mwaka 2014 na kuunda bunge lililojulikana kama Baraza kuu la kitaifa GNC. Bunge na serikali ambayo inaungwa mkono na jumuiya yakimataifa ilihamia upande wa mashariki mwa Libya.

Mwandishi: Isaac Gamba/ rtre/dpa
Mhariri: Iddi Ssessanga