Serikali ya Uingereza yaidhinisha kuuzwa kwa Chelsea FC
25 Mei 2022Matangazo
Waziri wa utamaduni, habari na michezo wa Uingereza Nadine Dorries amesema ametoa leseni inayoruhusu kuuzwa kwa klabu hiyo jana Jumanne, muda mfupi tu baada ya kupata idhini kutoka kwa wasimamizi wa ligi kuu ya Premia.
Dorries aliandika kwenye mtandao wake wa Twitter kuwa, wameridhika kwamba mapato yanayotokana na kuuzwa kwa klabu hiyo hayatamnufaisha Roman Abramovich ama watu wengine karibu yake waliowekewa vikwazo kutokana na uhusiano wao na mamlaka nchini Urusi.
Kampuni inayosimamiwa na Boehly, ambayo pia inamiliki klabu ya mpira wa Marekani ya Los Angeles Dodgers, ilikubali dau la pauni bilioni 4.25 la kuinunua Chelsea mnamo Mei 7.