1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Niger kizimbani kwa kuendeleza Utumwa

Scholastica Mazula9 Aprili 2008

Katika hatua ya Kihistoria, Mtumwa wa zamani ameishitaki Serikali ya Niger kuwa imeshindwa kutekeleza sheria zinazopinga utumwa.

https://p.dw.com/p/Df5d
Rais Mamadou tandja wa Niger.Picha: AP Photo

Mashitaka hayo yamefufua mgogoro kati ya Serikali inayopinga kuwepo kwa utumwa nchini humo na wanaharakati ambao wanasema Nchini Niger kunakutikana kiasi cha watumwa lakini nane.

Mahakama ya Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi-ECOWAS, inatarajia kupitisha hukumu ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Hadizatou mani Korau mwenye umri wa miaka 24.

kwa mujibu wa kiongozi wa kundi moja linalopinga utumwa nchini humola Timidria, Llguilas Weila, akiwa na umri wa miaka kumi na mbili, Korau alinunuliwa na mfanyabiashara kutoka kabila la Tuareg kwa thamani ya euro mia tatu sitini na sita sawa na dola mia tano sitini na saba na baadaye akanunuliwa kuwa mke wa tano wa mganga wa kienyeji huko Niger.

Hadizatou mani Korau ameiambia mahakama kuwa alikuwa akipata mateso makali kutoka kwa mganga huyo wa kienyeji ikiwemo kupigwa, kudhalilishwa na mara zote alikuwa akimkumbusha kwamba alimununua.

"Alikuwa ananipiga sana na ilinibidi kufanya kila aina ya kazi za nyumbani kwa ajili ya wake zake. Alikuwa akiniambia kuwa mimi ni mtumwa wake kwa sababu alininunua kwa hivyo ana haki zote za kunifanya anavyotaka lakini nimezaa naye watoto wawili".

Mwaka 2003 Niger ilipitisha sheria inayoutaja utumwa kua ni kitendo cha uhalifu.

Lakini kwa mujibu wa shirika la kimataifa linalopambana na utumwa,lenye makao yake mjini London,linalomuunga mkono kiongozi wa Timindria, viongozi wa mjini Niamey wanalaumiwa sio tu kwa kushindwa kumlinda Koarou asifanywe mtumwa,bali pia kwa kuhalalisha mtindo huo kupitia sheria za utamaduni na mila-sheria zinazokwenda kinyume na kanuni zinazohusiana na makosa ya jinai na katiba ya nchi hiyo.

Miko ya kuzungumzia utumwa nchini Niger ilivunjwa mwaka 2001,wakati mkutano wa shirika la kimataifa la ajira ulipoitishwa mjini Niamey ambako machifu walikiri kwamba shughuli za utumwa zinaendelezwa katika majimbo kadhaa ya nchi hiyo na kuahidi kupiga vita vitendo hivyo.

Bwana Weila anasema kwa miaka kumi sasa wamekuwa wakijaribu kuitahadharisha Serikali ya nchi hiyo kuhusu vitendo hivyo viovu.

"Tumekuwa tukiunga mkono hatua hiyo kwa miaka mitatu sasa, viongozi wetu wanapaswa kuelewa kwamba vitendo hivyo vinavyodharirisha utu wa mtu havihitajiki katika nchi hii".

Kwa miaka mitatu sasa msichana huyu amepeleka kesi yake mahakamani huko Konni, lakini mpaka sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na ndiyo maana tunajaribu kumsaidia ili kesi yake iende kwenye mahakama ya ECOWAS kwani amekaa kwa muda wa miezi mitatu jela kwa sababu ya kukataa kuendelea kuwa mtumwa".

Wakili mmoja wa Serikali ya Niger Mossi Boubacar, anasema Utumwa limekuwa jambo kubwa la kihistoria nchini humo.

Wachambuzi wa mambo wanasema endapo Mahakama itatoa hukumu dhidi ya kesi hiyo ambayo imekuwa ikisikilizwa tangu jumatatu, Aprili saba, itakuwa ni Uhai mpya kwa watu wa Niger wanaofanya kapeni dhidi ya Utumwa.

Wanasema endapo Mahakama itaiendesha kesi hiyo kwa lengo la kumsaidia Koraou, itaeleweka vibaya kwa Serikali ambayo siku zote imekuwa ikipinga kuwepo kwa Utumwa nchini humo na endapo haitafanya hiyvo itakuwa umelinyamazisha mdomo kundi la Timidria lisiweze kuendelea na kampeni zake dhidi ya Utumwa.

Serikali ya Niger imekuwa mara kwa mara ikijaribu kulinyamazisha kundi la Timidria ambalo jina lake linamaanisha Udugu, katika lugha ya Tamashek na limekuwa likitumiwa na jamii ya watu wa kabila la Tuareg katika kampeni hizo.

Bwana Weila, kiongozi wa kundi la Timidria, alifungwa jera mwezi Aprili mwaka 2005 kwa kujaribu kuandaa sherehe za ukombozi kwa Watumwa elfu saba walioko katika kambi ya Inates Magharibi mwa Niger karibu na mpaka wake na Mali.

Kufuatia kukamatwa kwa kiongozi huyo, Serikali ilisema imefanya hivyo kwa sababu kitendo hicho kingeweza kuungwa mkono na wanaharakati wa Kimataifa na hivyo kingechafua hadhi ya Niger ndani na nje ya nchi Ulimwenguni.

Makao makuu ya Mahakama ya Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi- yako mjini Lagos nchini Nigeria lakini inauwezo wa kufanya kazi zake katika nchi yoyote mwanachama wa ECOWAS endapo kutakuwa malalamiko yoyote na uwezeshwa wa kufanya jambo hilo.