Serikali ya mpito ya Ugiriki yaapishwa
17 Mei 2012Baraza hilo lenye mawaziri kumi sita linaloongozwa na kiongozi wa mahakama kuu ya Ugiriki Panagiotis Pikrammenos mwenye umri wa miaka 67, limeapishwa mapema leo kuiongoza Ugiriki kwa kipindi cha mpito. Hii ni baada ya baada ya uchaguzi wa mapema mwezi Mei kuibua mgogoro zaidi wa kisiasa na kuibua maswali kuhusu uanachama wa nchi katika ukanda unaotumia sarafu ya euro. Baada ya kuapishwa kwa baraza hilo la mawaziri, wabunge 300 wataapishwa na kuchukua nafasi zao kwa siku moja kabla ya bunge kuvunjwa tayari kwa uchaguzi mpya.
Wabunge hao walichaguliwa katika uchaguzi wa tarehe sita Mei, ambao hakuna chama chochote kilichopata kura za kutosha ili kuunda serikali. Mazungumzo ya kujarivu kuunda serikali ya umoja wa kitaifa yalikwama. Miongoni mwa wabunge watakaochukua nafasi zao wka siku moja ni 21 kutoka chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Golden Dawn, ambacho kinapinga nembo ya Wanazi mambo leo. Chama hicho kilifanya kampeni kikiahidi w´kuwafurusha nchini humo wahamiaji na kuvisafisha vitongoji vyao.
Wagiriki wakata tamaa
Wagiriki wengi wengi wako katika hali ya kukata tama baada ya miaka miwili ya kupunguzwa mishahara yao na marupurupu ya malipo ya uzeeni, hatua ambazo zimeshindwa kuleta manufaa ya kiuchumi ambayo yaliahidiwa na kusababisha maandamano makubwa nchini humo.
Chama cha siasa kali za mrengo wa shoto Syriza ambacho kinapigiwa upatu kushinda uchaguzi mpya, kinapinga mpango huo wa kubana matumizi kikitishia kuuchana mpango wa uokozi. Tsipras mwenye umri wa miaka 37 jana ameushutumu Umoja wa Ulaya na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kwa kile alichotaja kuwa ni kucheza kamari na maishja ya watu wa bara Ulaya.
Maafisa wa EU na IMF wameonya kuwa hakuna fedha zaidi zitakazotolewa ikiwa hatua zitakazopigwa kuhusu ahadi za mageuzi ambazo nchi hiyo ilitoa. Ugiriki inakumbwa na hatari ya kujiondoa katika kanda ya sarafu ya euro.
Mgogoro wa kisiasa wa Ugiriki umeifanya sarafu ya euro na masoko ya hisa barani Ulaya kuporomoka huku kukiwa na dalili ndogo kuwa uchaguzi mpya utakaofanywa tarehe 17 Juni utawezesha serikali dhabiti itakayotekeleza mpango mkubwa wa uokozi wa Umoja wa Ulaya – EU na Shirika la Fedha Ulimwenguni – IMF.
Waziri wa mambo ya Nchi za Kigeni wa Uingereza David Camerona amesisitiza mwito wake kwa viongozi wa kanda ya saarfu ya euro kuchukua hatua muhimu au mpango wake wa kuwa na sarafu moja uvunjike kutokana na mgogoro wa deni la Ugiriki.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Josephat Charo