1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Kenya imeteua wawakilishi katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki

31 Mei 2007

Hatimaye serikali ya Kenya imeteua wawakilishi wake katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

https://p.dw.com/p/CHDO
Uteuzi huo uligubikwa na vuta ni kuvute iliyochukuwa miezi sita baada ya vyama vya kisiasa nchini Kenya kutofautiana kuhusu atakayewakilisha nchi hiyo.Hatua hiyo ilipelekea kutoapishwa kwa wawakilishi wa mataifa mengine husika ya Uganda na Tanzania na kukwamisha shughuli za Jumuiya hiyo. Bunge la Afrika Mashriki EALA,lilifanya kikao chake cha kwanza mwezi Novemba mwaka 2001. Thelma Mwadzya alizungumza na Balozi Juma Mwapachu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Anaanza kuelezea walivyopokea taarifa hizo.