Serikali ya Ethiopia yatuhumu waasi kuzuia misaada
30 Machi 2022Katika taarifa, serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed hapo jana iliahidi kuwa inatumia kila mbinu kuwanusuru raia wake katika eneo la Tigray lakini haijapata ushirikiano wa upande wa TPLF.
Imesema msafara wa malori 43 ya chakula cha msaada kutoka mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa - WFP hayajaweza kuingia Tigray, kutokana na kufungwa kwa barabara ya Abala na waasi wa TPLF.
TPLF kwa upande wao wanasisitiza kuwa hakuna msaada wa kiutu uliowasili Tigray na kupinga ilichokiita ''madai ya uwongo'' yanayotolewa na serikali ya Ethiopia. Abiy Ahmed alitangaza mnamo Machi 24 mpango wa kusitishwa mapigano mara moja kwa muda usiojulikana ili kupisha msaada wa kiutu kupelekwa kaskazini mwa nchi. Waasi pia waliuridhia mpango huo lakini kipa upande ukatoa masharti.