1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali nchini Hungary imo hatarini

19 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDAr

Mji mkuu wa Hungary wa Budapest umeshuhudia maandamano makubwa kuwahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni. Maelfu kadhaa ya watu wamekusanyika mbele ya bunge la Hungary katika mji mkuu Budapest wakimtaka waziri mkuu Ferenc Gyurcsany kutoka chama cha kisoshialisti ajiuzulu. Kundi la waandamanaji wamevamia televisheni ya taifa na kusimamisha matangazo huku wengine wakiyachoma moto magari. Kulingana na taarifa zilizotolewa na televisheni asubuhi, watu 150 wakiwemo polisi 100, wamejeruhiwa katika ghasia ambazo zimezuka kati ya waandamanaji na polisi. Maandamano hayo yamefuatia kutangazwa jumapili iliyopita kanda ya radio ambamo waziri mkuu mwenyewe, alikiri kuwa alidanganya kuhusu mambo ya kiuchumi ili aweze kupata ushindi katika uchaguzi uliyofanyika mwezi Aprili mwaka huu.