Serikali Mpya ya Italia
14 Novemba 2011Matangazo
Waziri Mkuu wa mpya wa Italia Mario Monti amepewa jukumu la kuunda serikali baada ya Silvio Berlusconi kujiuzulu.
Rais wa Italia Giorgio Napolitano amearifu hayo baada ya kukutana kwa siku nzima hapo jana na wawakilishi muhimu wa vyama na wabunge.
Serikali mpya itakayoongozwa na Waziri Mkuu Mario Monti, mtu mwenye hadhi kubwa duniani ya utaalamu wa masuala ya uchumi itakuwa na jukumu la kuirejesha imani ya wawekaji vitega uchumi kwenye masoko ya fedha na kuindoa Italia kutoka kwenye mgogoro wa madeni.
Hapo jana baada baraza la Seneti, bunge pia liliupitisha mpango wa kubana matumizi ambao Italia inatakiwa iutekeleze na Umoja wa Ulaya.
.