Serikali mpya Italia kuapishwa leo
8 Mei 2008Matangazo
Roma:
Waziri mkuu mteule wa Italia Silvio Berlusconi amependekeza baraza lake la mawaziri la wajumbe 21, baada ya ushindi wa vyama shirika vya siasa za kati za mrengo wa kulia katika uchaguzi mkuu mwezi uliopita. Serikali mpya itaapishwa leo. Orodha ya mawaziri wa Bw Berlusconi ni pamoja na afisa wa ngazi ya juu wa masuala ya usalama katika umoja wa Ulaya Franco Frattini ambaye anakua Waziri wa mambo ya nchi za nje pamoja na Giulio Tremonti anayerudi kuwa waziri wa uchumi-wadhiafa aliokuwa nao katika serikali iliopita ya Bw Berlusconi 2001 hadi 2006.