Serikali kuu ya Muungano siku 100 Madarakani Berlin
26 Machi 2014Tunaanzia Berlin kumulika siku mia moja tangu serikali ya muungano wa vyama vya kihafidhina vya Christian Democratic Union-CDU,Chrisian Social Union CSU na wasocial Democrats wa SPD ilipoingia madarakani.Hawakuanza vibaya,hakuna malumbano hata kashfa ya Edathy haikuwatia kishindo au washirika wadogo SPD ndio wanaong'ara" ni miongoni mwa vichwa vya habari habari magazetini .Gazeti la "Münchner Mercur" linaandika:"Siku mia moja za muungano wa vyama vikuu zinabainisha wasoshial Democrat ndio walioshinda mashindano ya awamu hii ya kwanza madarakani.Hakuna aliyewapita:naiwe katika suala la malipo ya uzeeni,kiwango cha chini cha mshahara,malipo ziada kwa wazee au kuwekewa kikomo kodi za nyumba....Sote tunabidi tutambue kwamba tija ya uchaguzi wa leo,watoto na wajukuu zetu ndio watakaotakiwa wailipie kesho.Hapo serikali ina nafasi ya kurekebisha mambo sawa na vile inavyopaswa irekebishe katika suala la mageuzi ya nishati.
Mtaka cha Mvunguni huinama
Imani ya mnunuzi imepungua linapohusika suala la mazao ya "Bio" au yale mazao ambayo tangu mwanzo mpaka mwisho hayatumiliwi mbolea za sumu na kadhalika.Ili kutuliza hofu za wanunuzi na kurejesha imani,halmashauri kuu ya Umoja wa ulaya imetangaza sheria mpya.Gazeti la "Esslinger Zeitung" linaandika: " Ni sawa kabisa kuiona halmashauri kuu ya Umoja wa ulaya inawajibika na kutangaza viwango vya chini kabisa vya mabaki ya dawa ya kuuwa wadudu waharibifu katika mazao ya Bio.Kwamba baadae mazao hayo yanabidi yachunguzwe,si suala la kuulizwa! Usalama wa wanunuzi hauwezekani bila ya urasimu.Mtaka cha mvunguni huinama.Kila mmoja atabidi atambue ,akitaka "Bio" atabidi alipie " Bio".
Bayern Munich watawazwa kwa mara ya 24 mabingwa wa ligi kuu
Mada yetu ya mwisho magazetini inahusu kabumbu.Jana usiku timu mashuhuri ya Ujerumani Bayern Munich imevikwa taji la ubingwa wa ligi kuu -Bundesliga hata kabla ya michuano kumalizika.Gazeti la "Berliner Morgenpost" linaandika:" Kama ilivyokuwa ikitarajiwa,watoto wa FC Bayern Munich wamenyakuwa taji la mabingwa wa ligi kuu.Kwa wengi wa mashabiki wake lakini taji hilo la 24 katika historia ya Bayern Munich lilitiwa ila kidogo.Hata hivyo ni jambo la kawaida kwa kila kitu kutiwa ila humu nchini.Kuna wanaowamezea mate na wengine wanaowaonea kijicho.
Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman